Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema viongozi na watendaji watakaoitumia CCM kwa faida yao binafsi siku zao zitahesabika.

Polepole alisema chama hicho kitaendelea kuwa imara na daraja kati ya wananchi na serikali yao ili kuhakikisha kinawasemea watu wengi, maskini na wanyonge ambao haki zao zimeporwa na kupokwa kwa muda mrefu.

Pia Polepole amewataka viongozi na watendaji ndani ya chama hicho kuacha kukitumia kwa faida yao binafsi bali watangulize mbele maslahi ya wengi, vinginevyo siku zao zitahesabika.

Katibu huo alikuwa akizungumza na mabalozi na viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mkoa akiwa katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Ziara hiyo ina lengo la kumpongeza Rais John Magufuli kwa utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2025 pamoja na kuimarisha uhai wa chama hicho.

Naye katibu wa CCM mkoa wa Mwanza, Raymond Mwangwala alikemea mnyukano miongoni mwa watendaji wa serikali na viongozi wa kisiasa waliomo kwenye vyombo vya dola unaofukuta katika baadhi ya halmashauri mkoani Mwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *