Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Hamphrey Polepole amesema mchakato wa Katiba ulikwama kwa sababu hakukuwa na uelewa wa pamoja nini wananchi wanataka jambo ambalo, tayari limeshaeleweka ndani ya chama hicho.

Amesema yeye ni muumini wa maoni ya wananchi kwenye mchakato wa Katiba mpya iliyopendekezwa.

Amesema wakati ya mchakato wa Katiba mpya alikuwa miongoni mwa wajumbe waliokusanya maoni ya wananchi ataendelea kuunga mkono maoni yao.

Amesema mchakato huo ulikwama kwa sababu hakukuwepo na uelewa wa nini Watanzania wanataka.

Hata hivyo alidai kuwa mabadiliko makubwa yanayofanywa ndani ya chama hicho yanaakisi kushughulikia kero za wananchi.

Polepole amesema uongozi wa  Rais John Magufuli umejikita zaidi katika kushughulikia kero za wananchi kwa kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa uadilifu huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *