Katibu  wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM,  Humphrey Polepole amewashuru watanzania kwa kuipa ushindi CCM kwenye uchaguzi wa ubunge wa jimbo la Dimni Zanzibar pamoja Udiwani.

Kiongozi huyo amesema hayo leo katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

Mgombea wa CCM Juma Ali Juma ameibuka mshindi wa Ubunge jimbo la D Dimani ambapo pia chama hicho kilishinda katika kata 19 kati ya 20 ambapo moja imechukuliwa na upinzani.

Kata ambazo CCM imeshinda ni Nyarenanyuki (Arumeru, Arusha), Isegehe (Kahama, Shinyanga), Nkome (Geita), Kiwanja cha Ndege (Manispaa Morogoro), Lembeni (Mwanga, Kilimanjaro), Ihumwa (Dodoma), Matevez (Meru, Arusha), Kimwani (Muleba, Kagera), Igombavanu (Iringa), Kijichi (Mbagala, Dar es Salaam), Ng’hambi (Dodoma), Kinampundu (Singida), Kasansa (Katavi), Malya na Kahumulo (Mwanza), Mkoma (Mara), Misugusugu (Kibaha, Pwani).

CCM imeshindwa katika Kata ya Duru mkoani Manyara, ambako mgombea wa Chadema, Ali Shaaban ameibuka mshindi. Kwa upande wao, baadhi ya wasomi wamesema kwamba chama cha mapinduzi kimeshinda kutokana na kutekeleza ahadi za kuondoa kero za wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *