Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja baada ya kuumia misuli ya paja kwenye mechi ya klabu bingwa dhidi ya FC Basel siku ya jumanne.

Hilo lina maana kwamba huenda atakuwa na kibarua kujaribu kuwa sawa kucheza mechi ya Ligi kuu dhidi ya Liverpool ugenini 14 Oktoba.

Meneja wa United, Jose Mourinho anatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu hali yake katika kikao na wanahabari Ijumaa.

Pogba atakosa mechi za ligi dhidi ya Everton, Southampton na Crystal Palace, pamoja na mechi ya Kombe la Ligi raundi ya tatu Jumatano dhidi ya Burton.

Kadhalika, ataikosa mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ugenini dhidi ya CSKA Moscow mnamo 27 Septemba.

Aidha, atakosa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Bulgaria na Belarus mapema mwezi Oktoba.

Ufaransa wanahitaji kushinda mechi hizo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *