Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba leo ataukosa mchezo wa Manchestr Derby  baada ya kupata majeraha wakati wa mchezo dhidi ya Burnley wikiendi iliyo pita.

Kocha Mkuu wa Man United, Jose Mourinho amesema kuwa imeshindikana kwa Pogba kupona haraka maumivu ya nyama za paja alizoumia katika mchezo wa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Burnley.

Pogba alivyoumia kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Burnley wiki iliyopita.
Pogba alivyoumia kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Burnley wiki iliyopita.

Taarifa hizo ni mbaya kwa Manchester United kutokana na kuandamwa na majeruhi kibao kuelekea mechi za mwisho wa ligi hiyo ambapo wanawania kuingia nne bora kwenye msimamo wa ligi kuu.

Pogba anaungana na wachezaji wenzake waliokuwa majeruhi ambao ni Juan Mata, Phill Jones, Chriss Smalling, Marcos Rojo na Zlatan Ibrahimovich ambao pia wataikosa mechi ya leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *