Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amenunua nyumba ya kifahari yenye thamani pauni milioni 2.9, zaidi ya shilingi bilioni tano za kitanzania.

Nyumba hiyo ina vyumba vitano vya kulala, ikiwa na sehemu ya michezo mbalimbali na bafu kubwa la kisasa, milango ya joto, sehemu ya mkutano na waandishi wa habari na sehemu mbili za kupaki magari.

Baadhi ya vyumba kwenye nyumba hiyo.
Baadhi ya vyumba kwenye nyumba hiyo.

Nyumba hiyo ipo eneo la Cheshire ambapo wanaishi mastaa wakubwa nchini England. Kama mchezaji huyo atataka kutoka nyumbani kwake kwa gari kwenda kwenye Uwanja wa United wa mazoezi Carrington, basi atatumia dakika 20.

Pogba aliposajiliwa Manchester United alikuwa anakaa kwenye hoteli ya kisasa ya Lowry. na sasa ameamua kununua nyumba hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *