Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ameweka wazi kuwa kiungo wa Manchester United Paul Pogba, hana furaha ndani ya kikosi cha timu hiyo kutokana na kutokuwa chaguo la kwanza siku za hivi karibuni.

Pogba, mwenye umri wa miaka 25, yuko katika kikosi cha Ufaransa kitakachocheza mechi za kirafiki na timu za taifa za Colombia na Urusi.

Nyota huyo alitolewa kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Brighton Jumamosi.

Pogba aliachwa nje ya kikosi kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa Ulaya UEFA dhidi ya Sevilla na kisha kuachwa nje dhidi ya Liverpool kwa kile kilichoripotiwa kuwa ni majeruhi.

Pogba alirejea United mwaka 2016 akitokea Juventus kwa ada ya £ 89m na kuisaidia timu yake kushinda Kombe la Ligi pamoja na Europa League msimu uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *