Klabu ya Southampton imekamilisha usajili wa kiungo wa Morocco, Sofiane Boufal kutoka klabu ya Lile nchini Ufaransa kwa ada ya uamisho ya paundi milioni 16.

Boufal mwenye umri wa miaka 22 ameshinda magoli 11 kwenye ligi ya Ufaransa msimu uliopita na kuisaidia Lile kumaliza nafasi ya tano na kufanikiwa kucheza Europa League.

Baada ya usajili huo kukamilika mkuregenzi wa soka katika klabu ya Southampton amesema kwamba usajili huo ni mzuri kutokana na mchezaji huyo kuwa na uwezo wa hali ya juu ambapo aliuonesha wakatika akiwa ligi kuu ya Ufaransa.

Kwa upande wake kiungo huyo amesema kwamba anafurahi kujiunga na klabu hiyo na kusisitiza ataisadia kadri ya uwezo wake ili kuona timu hiyo inapata mafanikio iliyojiwekea msimu.

Kutoakana na usajili huyo unaifanya Southampton kuvunja rekodi ya usajili ndani ya klabu hiyo kwa kutoa kitita cha paundi milioni 16 ambapo mchezaji huyo amevunja rekodi ya Dani Asvaldo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 15 kutoka Roma Mwaka 2013.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *