Klabu ya Liverpool inawakaribisha Manchester United kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza itakayofanyika katika uwanja wa Anfield leo usiku.

Kwa upande wa Liverpool, mabeki Nathaniel Clyne na Dejan Lovren wamerudi huku Emre Can akitarajiwa kuanza kucheza kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kupona majeruhi.

Kwa upande wa Manchester United, kiungo wa Henrikh Mkhitaryan na beki Luke Shaw wako tayari kuelekea Anfiled baada ya kupona majeraha.

Huku beki wao Phil Jones ndio mchezaji wa pekee ambaye anauguza jereha katika kikosi hiko ambacho hakina majeraha mengi.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema mbali na jedwali la ligi ni mechi muhimu sana huku akisema anajua kuhusu historia ,napenda mechi maalum kama hizi. Kila mtu duniani ataitazama mechi hii.

Mechi hiyo itawakutanisha makocha wawili wakubwa dunia Jorgen Kloop kwa upande wa Liverpool na Jose Mourinho wa Manchester United.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *