Leicester City imepanda mpaka nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuicha Liverpool kwa mabao 3-1 kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa King Power.

Leicester walionesha kiwango cha juu, na magoli mawili kutoka kwa Jamie Vardy na moja kutoka kwa Danny Drinkwater yaliididimiza Liverpool.

Wakicheza chini ya kaimu kocha Craig Shakespeare, aliyechukua mikoba ya Ranieri, mabingwa hao wa England walicheza kama mabingwa watetezi.

Goli la kwanza la Jamie Vadry limekumbusha mtindo waliokuwa wakicheza msimu uliopita, baada ya pasi murua kutoka kwa Marc Albrighton iliyomfikia Vardy.

Magoli haya ya Leicester ndio magoli ya kwanza kwa klabu hiyo kufunga mwaka huu wa 2017.

Liverpool ambao wangeweza kupanda hadi nafasi ya tatu iwapo wangepata ushindi, sasa wamepoteza mechi tano kati ya saba walizocheza katika michuano yote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *