Everton imeshindwa kutumia uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Tottenham kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza iliyofanyika katika uwanja wa Goodson Park.

lukaku

Everton ndiyo iliyokuwa ya kwanza kujipatia goli lake kupitia kwa Ross Barkley mnamo dakika tano ya mchezo kufuatia faulo, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Everton walikuwa mbele kwa goli hilo moja.

Kipindi cha pili kilipoanza Tottenham ilionekana kutawala mchezo huo mpaka kupelekea kusawazisha goli hilo kupitia kiungo wake Erick Lamela katika dakika ya 59.

Mpaka dakika 90 ya mchezo huo zinamalizika timu hizo zilikuwa sare ya 1-1 na kupelekea kugawana pointi.

smith

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *