Pikipiki 16 zimetolewa matairi baada ya kukaidi agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dk. John Pombe Magufuli la kukataza magali ya kawaida na piki piki kutotumia bara bara ya mwendo kasi.

Rais Magufuli aliwaagiza jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kung’oa matairi vyombo vyote vya moto vitakavyopita katika barabara za mabasi yaendayo haraka kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema kuwa pikipiki hizo 16 zilizotolewa matairi ni sehemu tu ya nyingi zilizokamatwa huku akisema kuwa mkakati huo ni endelevu ambapo wote watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Rais Dkt Magufuli alitoa maagizo kwa askari kukamata magari na pikipiki zinazotumia barabara za mabasi yaendayo haraka na kisha kuzitoa matairi na madereva hao wafikishwe mahakamani.

Rais Magufuli alisema madereva hao wakiuliza matairi yao yalipo, wajibiwe kuwa askari hawajaajiriwa kulinda matairi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *