Beki wa Real Madrid na Uhispania, Sergio Ramos atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja baada ya kuumia goti kwenye mechi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Albania na Uhispania kushinda 2-0.

Ramos mwenye umri wa miaka 30 alitolewa kwenye mechi hiyo mnamo dakika ya 80 ya mchezo huo kutokana na maumivu hayo ya goti.

Klabu yake ya Real Madrid imethibitisha kwamba atakaa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja na atakosa mechi nne za La Liga ikiwemo dhidi ya Atletico Madrid.

Pia beki huyo wa kutumainwa wa Real Madrid atakosa mechi ya kombe la ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Legia Wazawa pamoja na mechi ya kufuzu ya kombe la dunia kati ya Uhispania na Macedonia Novemba 12 mwaka huu.

Sergio Ramos anakuwa mchezaji wa pili muhimu kuumia katika kikosi cha Real Madrid baada ya wiki iliyopita kiungo wa timu hiyo Luca Modrick kuumia na kukaa nje ya uwanjani kwa miezi kadhaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *