Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameonesha kukerwa na kitendo cha Zari ambaye ni mpenzi wake waliezaa nae watoto wawili.
Kumekua na picha zinazosambaa mitandaoni zikimuonyesha Zari akiwa ndani ya maji nusu uchi ambapo kwenye picha alizopost yeye Zari, alionekana mwenyewe lakini kuna nyingine zimesambaa zikimuonyesha akiwa na Mwanaume.
Diamond Platnumz ameonesha kuchukizwa na kitendo hicho na kuamua kuandika yafuatayo “Ndio maana wakati mwingine naonaga bora tu nile na kusepa…. maana hawathaminikagi wala kuaminika hawa“.
Dakika chache baadae, Zari alimjibu kuwa huyo ni mtoto wa Mjomba wake na kwamba picha hiyo aliipiga mke wa mwanaume huyo.
Pia Zari alisema kuwa, mwanamke ukiwa mwaminifu, mwanaume atatunga habari za uongo ili kufukia yale ambayo huyafanya wewe ukiwa haupo.