Mashabiki wa Bongo Fleva wamemjia juu, Ben Pol baada ya kuweka picha akiwa nusu uchi katika mtandao wake wake wa Instagram.

Mashabiki hao wameoneshwa na kuchukizwa na picha hiyo mpaka kupelekea kumtolea maneno machachu pamoja na matusi mara baada ya kuweka picha hiyo.

Staa huyo ameweka picha hiyo baada ya kuondoa picha zake zote kwenye akaunti yake hiyo ya Instagram kitendo ambacho kimewashangaza wengi.

ben-pol-1

Kwenye picha hiyo Ben Pol akuandika kitu chochote zaidi ya picha yenyewe na mwenyewe ajaelezea sababu ya kuweka picha hiyo katika mitandano ya kijamii.

Kutokana na picha hiyo kuanza kutrend katika mitandao ya kijamii mashabiki nchini wamejiuliza maswali ama kuna nyimbo anataka kutoa ndiyo mana kafanya hivyo iwe kama kiki yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *