Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bill Nass  anayefahamika kwa jina la Petit Man amefunguka aliyokutana nayo wakati alipokwenda lupango kituo kikuu cha Polisi (Centro) kwa tuhuma za dawa za kulevya.

Petit Man amesema kuwa kitendo cha kukaa mahabusu kwa wiki moja kimempotezea fedha nyingi ambazo alikuwa amepanga kuingiza kwa wiki ile ili kuwafikisha hatua nyingine wasanii wake wanaomtegemea yeye kwa asilimia kubwa.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa mahabusu si sehemu nzuri kwani amejifunza mengi sana na amekumbana na watu tofauti ambao wengine ameweza kuwasaidia na wengine imeshindikana.

Kwa upande mwingine amesema kuwa Wema Sepetu kuhama chama ni sawa kwasababu kila mtu ana mawazo yake na utashi wake hivyo kama ameamua kufanya hivyo, basi inabidi wao wawe wasikilizaji kwani Wema ana wazazi wake na kwamba hayo ni mapendekezo ya mtu.

Petit Man ni miongoni mwa watuhumiwa wa dawa za kulevya walitajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *