Mwanamuziki wa Nigeria kutoka kundi la P Square, Peter Okoye, ametakiwa kukamatwa na polisi baada ya kusemekana kuitukana serikali ya Nigeria kupitia kurasa yake ya Twitter.

Chama tawala huko Ngeria, APC kimelitaka jeshi la polisi kumkamata msanii huyo kwa kitendo ambacho wanadai kwamba PETER OKOYE ameitukana serikali.

Tatizo hilo limekuja baada ya Serikali ya nchini Nigeria kuwapiga marufuku wasanii kufanya video nje ya nchi ya Nigeria, na baada ya hapo Peter Okoye akaamua kutoa mawazo yake kuhusu sakata hilo.

Baada ya kutoa maoni yake hayo ndipo chama hicho nacho kikaja juu kudai kwamba msanii huyo ameitukana Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *