Mshambuliaji wa zamani wa West Bromwich Albion, Peter Odemwingie amedai kuwa yeye anaunga mkono kinachofanywa na mshambuliaji wa West Ham United, Dimitri Payet kwenye sakata la uhamisho.

Kwa sasa staa wa West Ham United, Payet amegoma kufanya mazoezi na timu hiyo na kulazimisha aruhusiwe kuhamia klabu ya Marseille ya Ufaransa.

Odemwingie aliwahi kupata umaarufu kwa kulazimisha asajiliwe na QPR akitokea West Bromwich Albion mwaka 2013.

‘Mimi binafsi ninaungana na mchezaji, kwasababu huwezi kwenda kinyume na klabu, uko peke yako’.

‘Kuna wakati ambapo klabu inatoa orodha ya wachezaji ambao haiwataki na hakuna shabiki ambaye anakutetea. Hawaonyeshi mapenzi na uaminifu kwa wachezaji ambao pengine wametoka kuwa majeruhi lakini wanachodhani ni kuwa timu inahitaji wachezaji bora zaidi’.

‘Na kuhusu Payet, amefanya vizuri katika timu na hakuna wanachopoteza na uamuzi wa busara unapaswa kufanywa kwasababu hata kocha wake Slaven Bilic amesema kuwa hali ya sasa si nzuri kwa yeyote kati ya pande zinazovutana’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *