Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Peter Msechu ametoa fursa kwa mashabiki wake kumuandikia nyimbo na kuzinunua.

Peter Msechu amesema kuwa ametoa furasa hiyo kutokana na muziki wake kwa sasa kuhitaji mchango wa watu wengi ili kuwa bora zaidi.

Mwimbaji huyo ameeleza kuwa mtu yeyote mwenye wimbo mkali amtafute na wakae chini kuongea kwa ajili ya kupatana bei.

Peter Msechu ambaye ni chumbuko la Bongo Star Search amesema kuwa yupo tayari kununua wimbo mmoja hadi milioni moja kutokana na ubora wa wimbo huo.

Msechu ameongeza kuwa toka awali alishaweka wazi kuwa yeye hajui kuandika nyimbo hivyo watu wasishangae kwani anafanya hivyo ili kuepuka kukurupuka kutoa nyimbo kama ilivyokuwa awali ila sasa hivi anajaribu kujipa muda.

Pia Peter Msechu amesema kuwa tayari ameshanunua wimbo mmoja na kuchajiwa milioni moja na aliyetunga wimbo huo, huku akibainisha wimbo huo atauachia baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *