Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kwamba mechi ya timu hiyo ya kufuzu kwa kombe la klabu bingwa Ulaya ni mechi muhimu zaidi msimu huu.

Kati ya klabu tano ambazo City huenda wakakutana nazo ni klabu ya AS Roma pekee ambayo ilikutana nayo katika mechi za makundi mwaka 2014-15 ikipata sare katika uwanja wa Etihad.

City ilipata ushindi wa mabao 2-0 katika uwanja wa Stadio Olimpiko kufuatia mabao ya Samir Nasri na Pablo Zabaleta na hivyo ikafuzu katika robo fainali ya michuano hiyo.

City imepangiwa kucheza dhidi ya timu ya Steaua Bucharest kutoka Romania kwenye hatua ya mtoano ya kombe la klabu bingwa Barani Ulaya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *