Mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa Paris Saint-Germain ‘PSG’ imemteua mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, Patrick Kluivert kuwa mkurugenzi wa soka wa klabu hiyo.

Kluivert aliyekuwa kocha wa kikosi cha chini ya umri wa miaka 19 cha Ajax ameamua kuiacha kazi hiyo na kujinga na kocha mpya wa Paris Saint-Germain, Unay Emery kwa ajiri ya kazi ya ukurugenzi.

Mshambuliaji huyo aliyewahi kutesa na timu za Ajax, Barcelona na Newcastle United aliwahi pia kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uholanzi chini ya kocha Louis Van Gaal.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *