Mgombea urais, Emmanuel Macron ameshinda Uchaguzi wa Urais wa nchini Ufaransa baada ya kupata asilimia.

Matokeo yanaonesha Macron amemuacha kwa mbali mpinzani wake Bi Marine Le Pen kwa kujinyakulia asilimia 65 ya kura.

Maelfu ya wanaomuunga mkono Macron walisherehekea katika kati mwa Paris wakipeperusha bendera.

Akiwa na miaka 39, Macron anakuwa rais waumri mdogo zaidi wa kuchaguliwa kuwahi kuiongoza Ufaransa na wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya vyama viwili vikubwa vya siasa nchini humo.

Katika taarifa yake, amesema kwamba Ufaransa imefanikiwa kufungua ukurasa mpya katika historia yake na kwamba alikuwa na ndoto ya kuwa mpiga mbiu wa nchi hiyo kwa kugunduliwa upya kwa matumaini na imani.

ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais Ufaransa

Emmanuel Macron, amenukuliwa akisema kwamba atahakikiksha anafanya kila linalowezekana kulipa fadhila ya uaminifu wa wafaransa waliompa.

Macron anasema ni heshima kubwa na mmenipa wajibu mkubwa wa kutekeleza, bila kauli yoyote kwangu, natoa shukrani zangu za dhati kutoka ndani ya moyo wangu.

Le Pen amempongeza Macron kwa njia ya simu na kusema kwamba chama chake cha National Front kimepata ushindi mkubwa kwa kugawana kura, na kufanikiwa kuigawa Ufaransa kati ya wazalendo na watawala.Wafuasi wa Macron wakisherehekea eneo la Louvre mjini Paris

Marine Le Pen aliyekuwa na matumaini ya kuikwaa nafasi ya rais wa Ufaransa tayari amekubali kushindwa dhidi ya mpinzani wake Emmanuel Macron.wa Macron wakisherehekea nje ya Louvre, Paris

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *