Pambano lililokuwa linasubiliwa kwa hamu kati ya bondia wa Uingereza, Amir Khan na Manny Pacquiao wa Ufilipini limeahairishwa.

Mabondia hao wawili walikuwa wametangaza pigano hilo kufanyika mnamo mwezi Aprili 28 katika mtandao wa Twitter mwisho wa mwezi Februari huku UAE ikitajwa kuwa eneo la pigano hilo.

Pigano hilo la mwezi Aprili lilipangwa baada ya mashabiki wa Paqcuiao katika mtandao wa Twitter kumpigia kura Khan kuwa mpinzani ambaye wangependelea bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 kupigana naye.

Khan mwenye umri wa miaka 30 aliyeshinda medali ya fedha katika uzani wa Lightweight katika michezo ya Olimpiki ya 2004, alimshinda Kell Brook, raia wa Australia Jeff Horn na Mmarekani Terence Crawford kwa asilimia 48 ya kura hizo zilizofanywa na Pacquiao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *