Bondia Manny Pacquiao ambaye pia ni Seneta nchini Ufilipino amevitembelea vikosi vinavyopambana na magaidi wa kundi la ISIS waliolivamia jiji la Marawi nchini humo.

Pacquiao alitembelea kikosi kilichoko katika eneo la Kusini mwa nchi hiyo majira ya saa tatu asubuhi (kwa saa za Ufilipino) akiwa amevalia sare za kikosi maalum cha jeshi la nchi hiyo ambacho kiliwahi kumtunuku ujumbe wa heshima wa kikosi hicho (honorary member).

Kwa mujibu wa Rappler, Pacquiao aliwatia moyo wanajeshi wanaopambana katika eneo hilo huku akieleza kuwa ana nia ya kujiunga na vikosi hivyo kusaidia mapambano.

Mapambano hayo yamesababisha zaidi ya watu 400,000 kuyakimbia makazi yao jijini Marawi na maeneo mengine ndani ya Ufilipino.

Vifo vilivyothitishwa na Mamlaka ya usalama nchini humo ni magaidi 630, raia 45 na wanajeshi wa Serikali 114.

Taarifa ya jeshi hilo kwa umma kuhusu ziara ya Pacquiao imeeleza kuwa imeviongezea ari vikosi hivyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *