Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa Bongo fleva, P Funk Majani amemwagia sifa mwanamuziki anayechipukia Harmorapa kwa ksema msanii huyo ni levo nyingine.

Toka msanii Harmorapa ameingia kwenye muziki kwa kuanza kujifafanisha na msanii Harmonize, kila wakati rapa huyo amekuwa akiingia kwenye ‘headline’ mbalimbali na kuzungumziwa na wasanii wengi wakubwa nchini, wengine wakifurahishwa na matendo yake.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na picha mbalimbali na Harmorapa mitandaoni zikimuonesha akiwa ameshikilia pesa nyingi jambo ambalo limemfanya producer huyo kuibuka na kumwagia misifa.

harmo-1

Kupitia akaunti yake ya Instagram P. Funk Majani ameandika “Chezea Harmorapa wewe!!! Levo zingine hizi”.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Usigawe Pasi’ inayoendelea kufanya vizuri.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *