Mastaa wa hip hop Marekani, P. Diddy na DJ Khaled wapo katika mazungumzo na Fox kwa ajili ya tv show mpya ya kusaka vipaji, “The Four,”.

Vyanzo vya habari vinavyoaminika vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa hakuna hata mmoja aliyesaini hadi sasa lakini mazungumzo yamefikia katika hatua nzuri.

Inaelezwa kuwa kutakuwa na majaji wanne ambapo Diddy atakuwa kiongozi, huku DJ Khaled ni mtayarishaji, pia kutakuwa na mwandishi wa nyimbo, na jaji  wa nne atakuwa upande wa utumbuizaji, pia katika nafasi hizo kutakua na mwanamke angalau mmoja.

Kipande kikuu cha show kitakuwa pop ila msisitizo zaidi ni katika hip hop. Itakuwa vita inayoendelea katika mtindo wa kuchanana mbele ya watazamaji na hatimaye mshindi atapatikana kutoka kwa majiji wote.

Hata hivyo hakuna taarifa show itakuwa wakati gani lakini inaeezwa kuwa na ladhaa ya tofauti na yenye kuvutia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *