Kocha wa Simba Joseph Omog, amesema kuwa atamkata mshahara mchezaji yeyote atakayechelewa kuripoti kwenye mazoezi ya timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambao umepangwa kuanza Desemba 17 mwaka huu.

Kocha huyo amesema amezungumza na wachezaji wote wakati akiagana nao kwenda kwenye mapumziko hayo mafupi hivyo hatokuwa na msamaha kwa yeyote ambaye atachelewa kufika mazoezini pasipo sababu za msingi.

Kocha huyo amesema wachezaji wote wa Simba ni profeshno, wanatambua majukumu yao na mikataba yao inavyoelekeza hivyo haoni sababu ya kupigizana kilele kwa sababu kila mtu anatambua wajibu wake kutokana na kanuni za klabu zinavyoelekeza.

Amesema kwa kutambua hilo ndiyo maana yeye kama kiongozi mkuu tayari, amewasili kwenye kituo cha kazi tayari kwa maandalizi hayo ambayo wanalazimika kuyafanya kwa umakini ili kutimiza kile ambacho wamekusudia kukifanya msimu huu nacho ni ubingwa.

Simba inalazimika kupambana kufa au kupona ili kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kupita katika kipindi kigumu cha misimu mitatu bila kutwaa taji lolote katika michuano yote iliyoshiriki ndani ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *