Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpo ameamua kuweka wazi suala la mahusiano yake kwa jamii baada ya kumuweka wazi mchumba wake ili watu wajue kama yupo nae.

Ommy alifunguka na kuthibitisha kuwa kwa sasa yupo kwenye mahusiano na raia wa China ambaye watu wengi hawamjui.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ommy Dimpoz ameweka picha ya pamoja akiwa na binti huyo mwenye asili ya China.

Ingawa Ommy Dimpoz hakutaka kufungua mjadala kwenye picha ile kwa kuamua kufunga uwanja wa comment ili watu wasiweze kuzungumza wala kujadili katika picha hiyo.

Lakini ukweli ni kwamba picha ile inazungumza mambo mengi kwa kila anayeiangalia kutokana na kuwa kimya sana kwenye uhusiano.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *