Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amekanusha taarifa za kuwa na mtoto nchini Marekani huku akisema kwamba bado hajajaliwa kupata mtoto kabisa.

Ommy amesema hayo baada ya kuulizwa kuhusu mtoto ambaye amekuwa akimpost kwenye instagram, kusema mtoto huyo siyo wake licha ya kuwa wanafanana.

Amesema kuwa “Mimi sina mtoto  kwa kweli yule ni mtoto wa rafiki yangu, kwa hiyo mimi kwake ni kama baba.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Sema nilivyopost na unajua sura zetu kidogo kama zinafanana, watu wakasema mtoto wa Dimpoz, mimi siwezi kujisingizia lakini kama Mungu akijaalia kama wangu atakuwepo wala sitaleta kona kona nitasema jamani mtoto wangu huyu”.

Ommy Dimpoz alipost picha akiwa na mtoto mdogo wa kike na baadhi ya watu wakidai ni wake lakini cha kushangaza msanii huyo aliifuta picha ya huyo mtoto ambaye ilikuwa katika ukurasa wake na kuacha video moja inayomuonyesha yuko naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *