Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesaini kufanya kazi na lebo ya muziki ya RockStar4000 nchini.

Lebo hiyo inafanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment.

Muimbaji huyo kwa sasa ataungana na Alikiba ambaye alijiunga na label hiyo miaka 6 iliyopita ambapo sasa nae ni mmoja wa wamiliki wa lebo hiyo.

Taarifa ya kusaini kwake kwenye lebo hiyo imesema kuwa “Tanzanian Superstar singer-songwriter Ommy Dimpoz signed global exclusive management deal with #ROCKSTAR4000 & content deal #RockstarTV at the Rockstar Pan Africa Group HQ in South Africa,”.

Ommy Dimpoz anaungana na wasanii wanzake ambao wapo chini ya lebo hiyo ambao ni Lady Jay Dee pamoja na Baraka The Prince.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *