Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya Bodi ya Baraza la CUF wanayomuunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif ya kutaka Msajili wa Vyama vya Siasa asitoe ruzuku kwa CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba.

 Maombi hayo namba 21 ya mwaka 2017 yametupiliwa mbali na Jaji Wilfred Dyansobera, baada ya Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata anayemuwakilisha mdaiwa wa pili Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kusema kesi imeitishwa kwa ajili ya uamuzi.

 Katika uamuzi maombi hayo ambayo mdaiwa wa kwanza ni Prof. Lipumba, Jaji Dyansobera amesema anakubaliana na moja kati ya pingamizi la AG kwamba vifungu vya sheria vilivyotumika kufungua shauri hilo sio sahihi.

 Hata hivyo, amesema anakubaliana na hoja za Bodi hiyo iliyo upande wa Maalim Seif kwamba suala la Bodi hiyo kutokuwa na uhalali linahitaji ushahidi wa kina.

 Aidha, kuhusu suala la Maalim Seif kusaini hati mbalimbali za shauri hilo bila kupewa mamlaka, amesema hilo sio pingamizi kwani mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa kuzingatia kiapo pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *