Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christopher ole Sendeka ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Sendeka anachukua nafasi ya Dk. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo akichukua nafasi ya Dk. Frolence Turuka aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Dk. Turuka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa balozi.

Wengine walioteuliwa na rais Magufuli ni Dk. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia mawasiliano, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Kamuzora ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *