Serikali ya awamu ya tano imetakiwa kuchunguza akaunti za viongozi wa Kamati za Bunge waliokuwa wakisimamia mashirika ambayo yamebainika kuwa yalikuwa yanajihusisha na vitendo vya ufusadi.

Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa NEC na Msemaji wa Chama cha Mapinduzi Taifa CCM Christopher Ole Sendeka na kuongeza kuwa uchunguzi huo ulinganishwe na mali wanazomiliki.

Kwa upande wa sekta ya mafuta amesema kuwa kuna haja kwa yale ambayo yameanzishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ya kuchunguza ubadhirifu wa mali na fedha za serikali.

Wakati huo huo Ole Sendeka amewataka waandishi wa habari kuacha kuandika habari za kichochezi kuhusu serikali ya awamu ya tano.

Kwa upande wa madai ya malipo ya wafanyakazi wa vyombo vya habari vya chama ambayo waliagizwa na Rais Dkt. John Magufuli kuyalipa amesema tayari wameshawalipa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *