Aliyekuwa mshambuliaji wa Nigeria na timu ya Bolton Wanderers ya Uingereza, Jay Jay Okocha amesema kuwa idadi ya juu ya wachezaji wa Kenya barani Ulaya itaipiga jeki timu ya taifa ya harambee stars.

Okocha amesema kuwa mchezaji wa Kenya Victor Wanyama anayechezea klabu ya Tottenham nchini Uingereza anaifanyia kazi nzuri Kenya na bara la Afrika.

Victor Wanyama
Victor Wanyama

Okocha amesema kuwa ni vyema mchezaji huyo anaipeperusha bendera ya Kenya juu na  kwa hatua hiyo inafaa kuwafungulia milango wachezaji zaidi wa Kenya kwenda Ulaya.

Amesema kuwa shirikisho la soka la Kenya linapaswa kuchukua hatua muafaka kwa lengo la kutumia fursa hiyo ili kuwasaidia vijana zaida kujiunga na klabu za Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *