Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa jumla ya mahakama za mwanzo 20 zinatarajiwa kujengwa jijini Dar es Salaam.

Makonda amesema kuwa kutokana na changamoto ya upatikanaji wa haki katika jiji hilo, wameamua kujenga mahakama hizo ili wananchi wengi waweze kupata haki kwa wakati kwa mujibu wa sheria.

Ujenzi wa mahakama hizo unasubiri ramani kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na utasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa pamoja na ujenzi wa mahakama hizo bado kuna tatizo kubwa la nidhamu na maadili ya watendaji wa mahakama.

Pia amesema kuwa uchache wa kesi katika mahakama ya mafisadi ndiyo mafanikio makubwa kwa hatua ya kuanzisha mahakama hiyo.

Vile vile Mwakyembe aliongeza kwa kusema kuwa  hatua ya Makonda kuanzisha utaratibu wa kuwatumia wanasheria vijana ambao watakuwa wanatoa elimu ya kisheria kwa wananchi mbalimbali ambao hawana uelewa juu ya sheria, ili iwasaidie katika kesi zao waweze kupata haki ni mzuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *