Swansea City imekataa dau la pauni milioni 10 lilitolewa na Everton ili kumsajili beki na nahodha wa timu hiyo Ashley Williams.

Beki huyo raia wa Wales alikua anakaribia kufikia makubaliano ya mwisho kwenda Goodison Park kujiunga na Everton.

Williams anamkataba na timu yake hiyo ambao unatarajia kumalizika mwaka 2018, msemaji wa klabu hiyo anasema hawako tayari kumuuza beki huyo.

4358858

Beki huyo ameichezea timu yake zaidi ya michezo 300 alisajiliwa kwa kiasi cha pauni 300,000 toka klabu ya Stockport mwaka 2008.

Everton wanasaka saini ya beki huyo ili kwenda kuziba pengo litakaloachawa na mlinzi wao mahiri John Stones anayehusishwa kutaka kujiunga na matajiri wa Man City.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *