Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza amefunguka na kusema kuwa kuanzia siku ya kesho hali haitakuwa kawaida nchini humo na kudai mambo yatabadilika kabisaa.

Odinga ambaye anapinga uchuguzi wa Rais ambao unaendelea leo nchini humo amesema kuwa kwanza watasusia bidhaa na huduma zote za kampuni zinazonufaisha udikteta nchini humo na kwenda mbali kuwa muungano wa NASA sasa utajulikana kama Muungano wa Kitaifa wa mageuzi.

“Kuanzia Ijumaa Oktoba 27, hali haitakuwa kawaida. Mambo yatabadilika kabisa, tutaleta pamoja makundi yote ya utetezi nchini kuhakikisha uchaguzi wa urais unaandaliwa upya kwa njia ya uwazi, haki na usawa katika siku 90. Tutasusia bidhaa na huduma zote za kampuni zinazonufaisha udikteta, tutaanzisha kampeni za kitaifa za kupinga mamlaka haramu ya serikali na kukaidi mashirika yake”.

Mbali na hilo Odinga amewataka wanachama na wapenzi wa NASA kutojihusisha na jambo lolote linalohusu Jubileee ikiwa pamoja na kushiriki uchaguzi wa leo na kusema zipo njia nyingi za kumuuwa panya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *