Kiongozi wa Muungano wa Upinzani Kenya NASA, Raila Odinga amesisitiza kuwa hakuna uchaguzi utakaofanyika siku ilipangwa na Tume ya Uchaguzi nchini humo Oktoba 26.

Odinga ameyasema hayo jana wakati akiwahutubia wafuasi wake jana eneo la Bondo  ambapo amewaambia kwamba hana imani kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

Aidha Bw Odinga amewataka Wafuasi wake wattulie n kumsikiliza kwabni atawapa maelekezo ya nini cha kufanya siku ya Jumatano ya Oktoba 25, ambayo itakuwa siku moja kabla ya uchaguzi.

Tumesema hakuna uchaguzi tarehe 26, wameanza kuleta jeshi hapa. Lakini sisi siyo wajinga. Kwa hiyo tarehe 25 mnisikilize kwa makini sana nitatoa ujumbe kwenu,”.

Uchaguzi huo wa marudio umepangwa kufanyika siku ya Alhamisi Oktoba 26 mwaka huu baada ya matokeo ya awali yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta kutenguliwa na mahakama kuu nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *