Kiongozi wa upinzani ya NASA nchini Kenya, Raila Odinga amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya IEBC, Wafula Chebukati.

Chebukati ambaye alikuwa akipingwa vikali na Raila amethibitisha kuwa wawili hao walizungumza kuhusu masuala ya uchaguzi ambao umekuwa tendawili.

Mwenyekiti huyo wa Tume alipendekeza kuwa mkutano unaofuata kati yao uhudhuriwe pia na Rais Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo, Rais Kenyatta amekataa wito huo wa Mwenyekiti wa Tume na kuendelea na msimamo wake kuwa kuwa uchaguzi mpya ulioelekezwa na Mahakama utafanyika kama ulivyopangwa.

Raila Odinga aliyetangaza kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho akipinga timu ya IEBC iliyosimamia uchaguzi wa Agosti 8 uliobatilishwa na Mahakama, ameendelea kuwataka wafuasi wake kuugomea uchaguzi mpya na kufanya maandamano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *