Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Peter Odemwingie amefungua milango ya maisha mapya ya soka nchini Indonesia kwa kujiunga na timu ya Madura United.

Odemwingie ambaye alikuwa mchezaji huru baada ya kuachana na timu ya Rotherham ya Uingereza amekubali kusaiini mkataba wa mwaka mmoja ukiwa na fursa ya kuongeza mwaka mwingine.

‘Hiki ni kipindi kinachovutia katika soka la Indonesia na ningependa kuwa sehemu ya kipindi hicho’. Odemwingine amenukuliwa na shirika la BBC

‘Natumai nitarudisha miaka nyuma na kufunga mabao muhimu kwaajili ya timu yangu’

Odemwingie amekuwa mchezaji wa tatu aliyewahi kuchezea ligi ya Uingereza kukimbilia Indonesia baada ya Michael Essien na Carlton Cole.

Msimu uliopita timu ya Madura United ilimaliza ligi ya nchini humo kwa kushika nafasi ya tatu.

Odemwingie ameichezea Nigeria mara 67 huku mechi yake ya kwanza ikiwa dhidi ya Kenya ambapo alifunga bao moja mwaka 2002 kisha alishinda medali ya shaba kwenye michuano ya Olimpiki ya mwaka 2008 huku akishika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya AFCON kwa mwaka 2004, 2006 na 2010.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *