Rais wa Marekani,Barrack Obama amewataka wamarekani wajizuie dhidi ya hisia kali baada ya mmarekani mweusi kuwapiga risasi na kuwaua polisi watatu wa kizungu katika shambulio la pili la kulipiza kisasi nchini humo.

Obama aliyasema hayo katika hotuba yake ya moja kwa moja kutoka Ikulu baada ya mmarekani mweusi kuwaua maafisa watatu wa polisi katika mji wa Boton Rouge nchini Marekani.

Obama amewataka wamarekani kuacha tabia ya kulipiza kisasi kwa sababu siyo suluhisho la tatizo la ubaguzi wa rangi nchini humo bali uchochea uhasama kati ya wamarekani weusi dhidi ya polisi wa kizungu.

Mji wa Dallas nchini Marekani ulikumbwa na machafuko baada ya polisi wa kizungu kuwaua wamarekani weusi bila kosa na mmarekani mweusi kulipiza kisasi kwa kuwaua maafisa watano wa polisi wa kizungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *