Rais wa Marekani, Barack Obama amevunja mkutano wake na Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Ufilipino.

Hapo awali Obama amesema kwamba angemuuliza kiongozi huyo maswali kuhusiana na mauaji ya kiholela ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa dawa za kulevya Ufilipino.

Duterte ambaye anaunga mkono mauaji hayo amesema iwapo hilo lingefanyika kwenye mkutano huo asingekubali kubadili msimamo wake kuwaua walanguzi wa dawa za kulevya nchini kwake.

Maafisa wa rais Obama wamesema badala yake kiongozi huyo sasa atakutana na rais wa Korea Kusini.

Msemaji wa baraza la taifa la usalama Marekani, Ned Price amesema kuwa Obama atakutana na Bi Park Geun-hye katika mkutano wa Mataifa ya Kusini Mashariki mwa bara Asia (Asean) mjini Laos ambapo viongozi wamekusanyika kwa mkutano mkuu.

Kampeni ya kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya ambapo washukiwa 2,400, wakijumuisha walanguzi na watumizi wameuawa nchini Ufilipino tangu achukue mamlaka mwezi Juni mwaka huu.

Ziara hii ni ya mwisho kwa Obama bara Asia akiwa kama rais wa Marekani ambapo sasa atkutana na rais wa Korea kusini.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *