Rais wa Marekani, Barack Obama amemsifu mgombea urais kupitia chama cha Democratic, Hillary Clinton na kusema ndiye anayefaa zaidi kuwa rais mpya wa Marekani.

Akihutubia katika kongamano kuu la chama cha Democratic lililofanyika katika mji wa  Philadelphia nchini humo, huku akishangiliwa na wajumbe.

Rais huyo amesema hakujawahi kuwa na mtu aliyehitimu zaidi kuongoza Marekani kuliko Bi Clinton.

Obama amemsifu pia kwa kujikakamua na kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya taifa hilo kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama kikubwa.

Amempongeza kwa kubomoa vizuizi na kuunda nafasi zaidi kwa Wamarekani huku akiwaahidi Wamarekani kwamba Bi Clinton anatetea umoja na maadili ya Wamarekani.

Obama: Akiwa na Hillary Clinton kwenye mkutano.
Obama: Akiwa na Hillary Clinton kwenye mkutano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *