Rais wa Marekani, Barack Obama amemtunuku makamu wake wa rais, Joe Biden Medali ya Rais ya Uhuru ambayo ndiyo nishani ya hadhi ya juu zaidi anayoweza kupewa raia nchini Marekani.

Biden alionekana kushangazwa na hatua hiyo baada ya kutokwa na machozi alipokuwa anatunukiwa medali hiyo.

Obama amemuelezea makamu huyo wa rais kwa imani yako katika Wamarekani wenzako, kwa upendo wako kwa taifa na kwa utumishi maisha yako yote.

Tuzo hiyo imetolewa kwa Bw Biden wawili hao wanapojiandaa kuondoka madarakani Donald Trump wa Republican atakapoapishwa kuwa rais mpya tarehe 20 Januari.

Baada ya kupewa meadli hiyo Biden amemshukuru rais Obama huku akisema kuwa anapanga kuendelea kushiriki siasa katika chama chake cha Democratic.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *