Rais wa Marekani, Barack Obama amemshutumu mgombea Urais nchini humo kupitia chama cha Republican Donald Trump kwa madai anayotoa kwamba kuna hila dhidi yake zinazofanywa katika uchaguzi nchini humo.

Amesema malalamiko ya mgombea huyo ni jambo ambalo halijawahi kutokea kwa mgombea nchini Marekani kujaribu kutilia shaka uchaguzi hata kabla haujafanyika.

Aidha Rais Obama amempa ushauri Mgombea huyo wa Republican ambaye ni mfanyabiashara tajiri Donald Trump kuendelea na kile anachokitafuta kuwa Rais ajaye wa Marekani.

Donard Trump
Donard Trump

Rais wa Marekani pia amemlaumu Bwana Trump kuonesha kwake kumsifu Rais wa Urusi Vladmir Putin na sera zake kufuata za kiongozi huyo.

Kampeni za Uchaguzi nchini Marekani zimekuwa zikifanyika katika hatua za lala salama, ikiwa imebaki siku chahe kufanyika kwake. huku Donald Trump akiendelea kuwaambia wafuasi wake kwamba serikali ya nchi hiyo, imekuwa ikimchafua lakini atashinda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *