Nyumba ya aliyekuwa nahodha wa timu ya uingerewza, John Terry imevamiwa na watu wanaodhaniwa ni majambazi na kuiba baadhi ya vitu wakati akiwa katika likizo ya kifamilia.

Maafisa wa polisi wa Surrey walithibitiha kwamba nyumba iliopo Oxshott ilivunjwa wikendi iliopita.

John Terry ameripotiwa kuishi katika nyumba ya vyumba saba nchini humo ambayo ilivamiwa na majambazi.

Msemaji wa kituo hicho cha polisi wa Surrey amesema kuwa  “Tunaweza kuthibitisha kuwa wizi ulifanyika katika nyumba moja iliopo Moles Hill ,Oxshott usiku wa terehe 25 na 26 mwezi Februari”.

Wezi hao wanadaiwa kuvunja na kuuingia katika nyumba hiyo na kuiba vitu vyenye thamani wakati ambapo mchezaji huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 36 alikuwa ameenda likizo na watu wa familia akiwemo mkewe Toni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *