Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu amesema kuwa amerudi jijini Nairobi kuratibu safari ya Tundu Lissu kwenda Marekani kwa matibaba zaidi.

Nyarandu amethibitisha hayo kupitia akaunti yake ya Facebook baada ya kuwasili jijini Nairobi ambapo anatarajia kushirikiana na baadhi ya wabunge wa Chadema kumsafirisha Tundu Lissu.

Kupitia akaunti yake ya Facebook ameandika ”Tumekuwa NairobiHospital tukisubiri MADAKTARI watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh TunduLissu kwa minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh Tundu Lissu kupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE”.

LAKINI bado KALAMU zao ni nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe.

Pia ameongeza kwa kuandika “Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya uwezekano wa kumhamishia Mh TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora zaidi, endapo MADAKTARI wa NairobiHospital wangeridhia.

Mwisho amemaliza kwa kuandika “Kesho asubuhi nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI hiyo”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *