Mkali wa wimbo Jike Shupa, Nuh Mziwanda ameamua kuuaga ukapera baada ya kufunga ndoa kimyakimya na mpenzi wake wa muda mrefu aitwae Nawal.

Ndoa ya Nuh na Nawal imewashtua wengi kwa kuwa hakukuwa na taarifa ambazo pengine watu walitegemea zingesambaa mitandaoni kuhusu lini angefunga ndoa hiyo kama ambavyo hufanya wasanii wengine, lakini cha ajabu watu wamekutana na picha mitandaoni zikionesha tayari Nuh amekwishafunga ndoa na Nawal.

Inasemekana kwa sasa Nuh na Nawal wanajiandaa kufanya bonge la party kusherehekea ndoa yao mpya.

Mastaa wengine waliofunga ndoa hivi karibuni ni pamoja na Masanja Mkandamizaji, Nyandu Tozzy, Tunda Man, Mabeste pamoja na Mwana Fa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *