Mkali wa wa ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda ameingia katika mgogoro na aliyekuwa meneja wake, Petii Man kutokana na madai kuwa  meneja huyo amekuwa akitumia jina lake vibaya kupiga hela.

Nuh amesema Petii Man alikuwa ni mpigaji, na hakuwa na mchango wowote katika kuuendeleza muziki wake, huku akimkumbuka mpenzi wake wa zamani kwa kusema “Mtu wa kumshukuru katika muziki wangu ni Shilole na si Petit Man”.

Nuh aliongeza kwa kusema “Nilishapoteza miaka mitatu kwa ishu za mapenzi sasa siwezi kupoteza mwezi mmoja kwa mtu ambaye hana mchango wowote kwangu na kanikuta tayari nimeshakuwa star, siwezi kufanya kazi na yeye kwa sababu hatuendani na anachukua hela kupitia mgongo wangu bila mimi kujua na pia ni meneja ambaye yeye anahangaika zaidi yeye mwenyewe kuwa star”.

Kwa upande mwingine Nuh alitambulisha Studio yake mpya aliyoipa jina la L.B RECORDS aliyoizundua hivi karibuni.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *