Staa wa Bongo fleva, Nuh Mziwanda amesema kwamba wazo la nyimbo yake ya “Jike Shupa” alilitoa Alikiba mbaye alimshirikisha kwenye wimbo huo unaosemekana amemuimba aliyekuwa mpenzi wake, Shilole.

Staa huyo amesema hakuwa na wazo wa jina hilo mpaka alivyomwambia Alikiba kuhusu hiyo nyimbo ndiyo Alikiba akaamua kuipa jina la “Jike Shupa”.

shupa

Nuh amesema AliKiba ndiyo kila kitu, yeye ndiye aliyetoa neno la “Jike Shupa” lakini alimkuta ameshaurekodi na ameshafanya chorus  na hakutaka kuiachia ndiyo akaenda kumshirikisha AliKiba.

Wimbo huo umefanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na TV nchini na  kumtambulisha rasmi Nuh Mziwanda katika muziki wa bongo fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *